Home music Mama D, Mobeto Wafukua Makaburi

Mama D, Mobeto Wafukua Makaburi

517
0

BAADA ya mwanamitindo Hamisa Mobeto naye kumpeleka mwanaye, Abdul Nasibu ‘Dyllan’ kwa baba yake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, mapya yameibuka.

 

Kitendo hicho kimefukua makaburi ya lile bifu kati ya Mobeto na mama mzazi wa Diamond au Mondi, Sanura Kassim ‘Mama Dangote’.

 

Inasemekana kwamba, Mama Dangote hakufurahishwa na kitendo hicho kwa sababu hakuwahi kumkubali Mobeto tangu zamani.

 

Watu wa karibu wamelieleza IJUMAA WIKIENDA kwamba, tofauti na ilivyokuwa wazazi wenza wengine wa Mondi, Zarinah Hassan ‘Zari’ na Tanasha Donna ambao walipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Mama Dangote ambaye wakati hao wanakwenda nyumbani kwa mwanaye huyo, Mbezi-Beach jijini Dar, mama huyo alikuwepo kuwapokea wajukuu wake, lakini safari hii hakuonekana.

Hata hivyo, wakati Dyllan akiwa nyumbani kwa Mondi, ndugu wengine wote akiwemo dada wa jamaa huyo, Esma Khan ‘Esma Platnumz’ walimposti mtoto huyo akiwa amepozi kwenye kabati la tuzo za baba yake, lakini Mama Dangote hakufanya hivyo na badala yake akamposti Tiffah Dangote na kumuita Mama Dangoengaa.

 

Ishu hiyo inatajwa kufufua vita mpya ya maneno kati ya Team ya Mobeto (Team Hamisa) na ile ya Mama Dangote (Team Mama Dangote).

 

Baadhi ya Team Hamisa walimfuata mama huyo na kumtaka aache roho mbaya, amfurahie Dylan kama alivyofana kwa wajukuu wake wengine.Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Mama Dangote, Mobeto alisema hana cha kusema.

Previous articleNew Gospel Audio :Jennifer Mgendi – Nakuachia Uwanja |Mp3 Download
Next articleNew Video :Rayvanny – Kiuno | Mp4 Download

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here